Video ya Diamond ‘Number One Remix’ yafikisha views milioni 10 Youtube
Miongoni mwa vipimo vya mafanikio kwa mwanamuziki yeyote duniani ni pamoja na namba, ndio maana ni muhimu sana kwa msanii kuhakikisha ana namba zinazoshawishi katika mitandao yake ya kijamii kwa maana ya followers, na views za kutosha Youtube.
Diamond Platnumz anaendelea kuthibitisha ukubwa wake, video yake iliyomfungulia njia za kimataifa ‘Number one Remix’ aliyomshirikisha Davido imetazamwa mara 10,003,353 hadi leo August 20. Iliwekwa Youtube Jan 6, 2014.
Diamond amewashukuru mashabiki wake kwa kuandika;
“Watazamaji zaidi ya Milioni kumi 10M, nawashkuru sana… amini si mimi ni Nyinyi na mimi ndio kwapamoja tunakuza Mziki huu…InshaAllah Mwenyez Mungu atusmamie tuzidi fika Mbali…Tuseme Amen.”
Post a Comment